Lagos - Maputo 2018: Wito wa Kushiriki

06 March 2018 | by Emeka Okereke

Kwa zaidi ya miaka 8, Invisible Borders Trans-African Organization imefanikiwa kwa kiwango cha hali juu kuratibu miradi saba ya Safari za kisanii iliyosaidia kushajiisha kubadilishana mawazo na sanaa kati ya nchi na wasanii wa Afrika kwa kupitia mipango mbambali ya kisanii.
Miradi hii kwa kiwango kikubwa imesaidia wasanii kusafiri kutoka Lagos kwenda sehemu nyingine za Afrika. Hata hivyo, katika mwaka 2014, mpango mpya ulianzishwa ambapo Usafiri kati ya Mabara uliandaliwa.

Washiriki walisafiri kwa kutumia barabara kutoka Lagos Nigeria mpaka Sarajevo, Bosnia. Mwaka 2016,  Mradi uliamua tena kutazama ndani ya bara la Afrika na nchi ziilizopo, hii ilisaidia kuzaliwa kwa Border Within/ Mipaka ya Ndani. Kati ya mwaka 2016  Na 2017 kuliikuwa na matoleo mawili ya Border Within/Mipaka ya Ndani na mipango yote miwili ilikuwa ni Safari za ndani za Nigeria.

Mwaka 2018, Mradi wa Invisible Border Trans-Africa unaingia katika toleo lake la 8 la safari zake za kisaniii.  Safari hizi za barabarani kwa wakati huu, zitatazama zaidi kusafiri ndani ya mipaka ya nchi za afrika ambapo nchi, miji, vijiji, mito na Nja kuu zinazounganisha nchi za afrika kati ya Lagos (Nigeria) na Maputo (Msumbiji) zitatumika ndani ya kipindi cha siku 95, kutoka Agusti 20 mpaka Novemba 23, 2018.

Safari hii itawajumuisha washiriki 21 kwa pamoja. (watendaji 3, Washiriki-Watakaovuka mipaka ya nchi 9, na Washiriki-Waalikwa 9)

Kama ilivyoikuwa methodolojia  katika safari zilizopita, washiriki wa safari za Invisible Bourders Trans-Africa Road kwa mara nyingine tena, watatumia miili yao, kama sehemu ya kuzalisha mawazo mapya, kujadili na kutengeneza tafakuri mpya kuhusu mipaka katika mantiki nzima ya safari.

Kupitia mambo halisi, hadithi na matukio ya maisha ya kila siku, barabarani na katika mipaka kati ya nchi na nchi, Wasanii watapata ujuzi ambao utatumika katika maeneo yao husika ya ubunifu ili kuwakilisha wakati safari ikiendelea, uwakilishi utakuwa moja kwa moja katika jamii watakayokutana nayo ama kupitia mtandaoni (tovuti na blogu) .

Jinsi ya Kutuma Maombi:

Tunatafuta wasanii wa Afrika wenye shauku na sanaa (wapiga picha, waandishi, watengenezaji sinema, wanahistoria, wasanifu majengo, wacheza ngoma, wasanii wa sanaa za majukwaani, na wasaniii wa grafiti) ambao wanapenda kuwa sehemu ya safari hii. Kama una shauku ya kushiriki katika mradi huu, tafadhali jaza fomu HII.  Vilevile yakupasa kusoma vigezo zaidi vinavyohitajika na mpango mzima wa safari ya mwaka 2018 HAPA .

KAMA UTAPENDA KUTUMA MAOMBI, TAFADHALI JAZA FOMU HII YA MAOMBI

Muhimu kufahamu, kwamba safari ya mwaka 2018 inatazama zaidi ya kipaji, ustadi,  na tajriba ama uzoefu-kwa kuelewa kwamba juhudi zozote za kisanii zitategemea na matukio na safari yenyewe. Kwa hivyo basi washiriki, mara baada ya kuchaguliwa, wataanza mara moja kufanya tafiti, kukusanya na kuchangia matokeo ya tafiti zao mahsusi kwa utaratibu wa safari miezi michache kabla safari yenyewe haijaanza.

Vivyohivyo ni muhimu sana kwa washiriki watarajiwa kufahamu kwamba kwa kutegemea na ufadhili utakaopatikana, Invisible Border itagharamia usafiri (Usafiri wa anga na usafiri wa ndani), malazi kwa wasanii wote na posho ya siku. Hata hivyo, kama kutakosekana ufadhili utakaotosheleza gharama zote, wasanii wataombwa kujigharamikia wao wenyewe posho za kujikimu na usafiri wa ndege mpaka eneo husika ambapo safari itaanza. Invisible Bourder itawasilisha utaratibu wa mwisho wa ushiriki kwa washiriki kabla ya safari haijaanza ili kuwa pa nafasi nzuri ya kujiandaa.

Miongozo:

  • Tafadhali, hakikisha unasoma maelekezo kwa ufasaha kabla ya kujaza fomu ya maombi ama kutuma nyaraka zinazohitajika, kwani hatutashughulika na maombi yoyote ambayo hayatafuata maelekezo yaliyotolewa.
  • Ili kutuma maombi, lazima uwe ni Mwafrika (makazi yako Afrika ama nje ya Afrika) muhimu zaidi ni kuwa pasi ya kusafiria kutoka katika moja ya nchi za Afrika. Kama  hauna pasi ya kusafiria kutoka katika nchi mojawapo ya Afrika, inakupasa katika  barua yako ya maombi kutoa maelezo kuhusu asili na uhusiano wako na Afrika.
  • Inakupasa kutuma maombi kama Mshiriki-mwalikwa au Mshiriki-Atakayevuka mipaka ya nchi zilizochaguliwa.
    • Washiriki-waalikwa ni wasanii ambao watashiriki ndani ya mipaka ya nchi zao ambapo safari hii itapitia.
    • Washiriki-Watakaovuka mipaka ya nchi ni washiriki watakaosafiri ndani na na nje ya mipaka ya nchi zilizopo katika msafara huu na watakuwa katika bechi/makundi mawili.
      • Bechi/Kundi A (Safari kutoka Lagos mpaka Kampala kutoka Agosti 20-)
      • Bechi/Kundi B (Safari kutoka Kampala mpaka Maputo)
  • Waombaji watakaochaguliwa wanaweza pia kubadilishwa kama ushiriki wao wa mipango ya awali ya safari hautakidhi matakwa/masharti ya mradi. Kama ambavyo imeainishwa katika tangazo, safari hii itakuwa ni kubwa, hivyo basi kuna umuhimu wa kufanya maandalizi ya hali ya juu kabla ya safari husika.
  • Muhimu sana kwa Wasanii watakaomba kama Washiriki-Watakaovuka mipaka ya nchi kuwa na pasi halali ya kusafiria (kuisha zaidi ya Miezi 2 baada ya safari) kabla ya ufanya maomi.
  • Waombaji wenye nia ya kushiriki kama Washiriki-Waalikwa lazima wawe ni Wasanifu Majengo, Wasanii wa grafiti, Wasanii Waigizaji, Waandishi, Wacheza ngoma, Wapiga picha ama Waandaaji wa Sinema.
  • Waombaji wenye nia ya kushiriki kama Washiriki-Watakaovuka mipaka ya nchi lazima.
  • Waombaji wote wenye nia ya kushiriki kama (Washiriki watakaovuka mipaka ya nchi (Tran-Border participants) wanatakiwa wawe na muda (wa siku zote 95) za mradi kwa kuwa washiriki watakaochaguliwa watakuwa katika makundi yatakayopangwa kutokana na mahitaji ya mradi.
  • Ili kuepuka mkanganyiko wowote utakaojitokeza, waombaji wote wanatakiwa waandike majina yao kwa ufasaha kabla ya kutuma maombi yao.

Mwisho wa maombi haya: Usiku, 16 Machi, 2018
Safari:Kama una maswali, wasiliana na info@invisible-borders.com.

 

Dokezo: Ukiachia kutoa maelezo kuhusu kazi zako na zina uhusiano gani na muktadha mzima wa mradi, tutapenda kwa ufasaha kabisa kulezea sababu zilizokufanya ukachagua kuomba kushiriki katika safari hii na vilevile ueleze kwa ufasaha  jinsi utakavyo changia utendaji wa kundi zima wakati ambao utakuwa na jukumu la  kubuni na kutengeneza kazi zako vilevile ukiwa katika siku zote ukishiriki  safari hii na washiriki wengine.

bShare on Facebook
aShare on Twitter
dShare on Pinterest